MAFUNZO VIJANA WAKATOLIKI MARA

Vijana wa kanisa Katoliki na madhehebu mengine mkoani Mara wameaswa kujenga utamaduni wa kujisomea  na kujielimisha juu ya mambo na taarifa mbalimbali za kijamii hususani juu ya masuala ya matumizi sahihi ya huduma za nishati na maji zikiwemo bei elekezi zinazotolewa na malmaka husika kupitia machapisho na vyanzo mabalimbali vya habari ili kuweza kuisaidia jamii wanamoishi juu huduma hizo muhimu kwa maisha ya kila siku.
Ushauri huo umetolewa na wawezeshaji  katika mafunzo kwa vijana wapatao 150  wa Madhehebu mbalimbali na misikiti yaliyoandaliwa na Baraza la ushauri  la watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC) yalifofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa manispaa ya Musoma mkoani Mara ambayo yalilenga kuwaelimisha vijana  juu ya haki na wajibu wa matumiaji wa huduma za nishati na maji, namna ya kuwasilisha malalamiko endapo mtumiaji ameathirika kwa namna yeyote ile na huduma iliyotolewa na mtoa huduma pamoja na matumizi sahihi na ya huduma za nishati na maji majumbani.
Katika mafunzo hayo vijana walielimishwa namna nzuri ya matuzimi sahihi ya nishati za umeme majumbani katika kuokoa gharama zisizokuwa za lazima, matumizi sahihi ya maji na ujazaji salama wa mafuta ya petrol katika magari na pikipiki sambamba kutoa malalamiko yao pale wanapopatiwa huduma isiyokidhi ubora kwa mamlaka husika na ikibidi kudai fidia endapo mtoa huduma amesababisha hasara au kuathiri mtumiaji huduma.
Kwa upande wao vijana hao wametoa kero zao kwa watoa huduma hizo Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira MUWASA kuwa kumekuwepo na kauli na lugha zisizo za kulidhisha kwa wateja pindi wanapofika kutoa malalamiko yao kwenye ofisi za mamlaka huku mwakilishi wa MUWASA kwenye mafunzo hayo CHAUSIKU JOSEPH akiahidi kulifikisha na kulishughulikia suala hilo kiofisi ili kutatua kero hizo ambazo zilielekezwa katika mamlaka hiyo.



Kwa upande mwingine vijana hao walielekeza malalamiko yao shirika la umeme TANESCO mkoani Mara kwa kutoa taarifa za katizo la umeme kwa maeneo ya mijini tu kwani magari ya matangazo yamekuwa yakipita maeneo ya katikati ya miji hususani barabara za lami na wananchi waliopo pembezoni mwa mji wa Musoma kutofikiwa na magari hayo ya matangazo na wananchi kutopata taarifa ya kuwa huduma ya umeme hautakuwepo na hivyo kukwamisha shughuli za kiuchumi na huduma zingine kama maandalizi ya usagaji na nafaka kwa ajili ya chakula majumbani huku mwakilishi wa shirika hilo kwenye mafunzo JAMES VESSO akiahidi kulishughulikia.
Mafunzo hayo ya siku moja ni mara ya kwanza kushirikisha kundi la vijana kutoka madhehebu mbalimbali na misikiti mkoani Mara na wawezeshaji wake ni  Rick Marwa, Peter Adam , Sekunda Ndamalya na Robinson Wangaso ambao ni wajumbe wa kamati ya mkoa wa Mara ya ushauri  ya watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA RCC )na Getrude Mbiling’i  kutoka  Baraza taifa ambao katika mafunzo hayo walisisitiza dhana nzima ya ushirikiano na mahusiano baina ya watoa huduma na watumiaji wa huduma kwa maana ya wananchi.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Comments