"VIJANA MUWE NA MSIMAMO"


Askofu wa Jimbo Katoliki MTWARA Mhashamu TITUS MDOE, amewataka  
Vijana wa Jimbo Katoliki MTWARA pamoja na Vijana wengine wote  kuwa na msimamo wa Kiimani kwa kumfuata KRISTO na kuyafanya yanayopendeza katika jamii.

Askofu MDOE ametoa wito huo katika homilia yake wakati akiadhimisha Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya Matawi iliyofanyika Parokia ya Kanisa Kuu parokia ya Watakatifu Wote Jimboni MTWARA, ambapo ilienda sanjari na siku ya 33 ya Vijana Ulimwenguni.

Amesema kuwa, Vijana wanapaswa kujitambua katika maisha yao wanayoishi, ikiwemo kumkumbatia KRISTO, kusimamia miongozo ya Imani, kulitunza na kulipenda Kanisa, kwani pasipo kufanya hivyo watabaki katika mahangaiko, huku wakikumbana na changamoto nyingi za kimaisha.

Aidha Askofu MDOE amewaomba Wazazi na Walezi kuwa mstari wa mbele, katika suala zima la malezi kwa vijana wao, ili kutengeneza jeshi imara lenye misingi bora ya kumjua na kumfuata KRISTO.

Comments