Na
Getrude Madembwe, Iringa.
Askofu wa Jimbo Katoliki Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini kumuombea
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli na serikali yake ili waweze kuliongoza Taifa kwa haki
na Amani.
Aidha
amewataka pia waamini hao kuombea hali
njema ya hewa ili mazao yaliyo mashambani yaweze kustawi vizuri sababu mazao
mengine bado madogo na yanahitaji mvua.
Askofu Ngalalekumtwa ameyasema hayo wakati wa homilia yake kwenye misa takatifu ya
Pasaka katika Kanisa Kuu la Moyo Mt. wa Yesu Parokia ya Kihesa na kuhudhuriwa
na watawa kutoka mashirika mbaimbali yaliyopo jimboni hapa na waamini wenye
mapenzi mema.
“
Amani tuliyonayo ni tunu kutoka kwa Mungu hivyo watanzania tunapasika kuilinda,
tumuombee pia Rais wetu na serikali yake ili iwe yenye huruma na inayoongoza
kwa kufuata msingi ya haki.” amesema mhashamu Ngalalekumtwa.
Mhashamu
Ngalalekumtwa amesema kuwa, pasaka ni karamu ya upole, wema ni kuhama kutoka
penye hali mbaya ya kuwa mnyonge ili waweze kuishi mbali na utumwa wa
ibilisi.
“Pasaka
hii inatufundisha kutendeana mema, wema kwamba tunapoadhimisha pasaka watafute
haki, watafute Amani kwa kila mmoja wetu atambue na aone kuwa mwenzake
anastahili kulindwa na kutendewa haki ma kusaidiwa kukuza karama zile
alizojaliwa na Mungu, wadogo na wanyonge wapewe upendeleo katika akili zao na
ndipo Mungu wetu atakapotukumbatia ikiwa watawakumbatia wanyonge na wenye shida.”
amesema Askofu Ngalalekumtwa.
Amewataka
waamini hapo pia kuombea ustawi wa Imani yao na hasa kwa kipindi hiki
wanapomshukuru Mungu na kuelekea kuadhimisha miaka 150 ili ionekane miaka
hiyo imewapeleka pazuri

Comments
Post a Comment